Akaunti zote za WhatsApp zimeungana na namba za simu rununu. Kwa kuwa ni kawaida kwa namba za simu kutumiwa tena na watoa huduma za rununu, inawezekana kwamba mmiliki wa zamani wa namba yako ya simu alitumia WhatsApp.
Ikiwa mmiliki wa zamani wa namba yako ya simu hakufuta akaunti yake ya WhatsApp, wewe na waasiliani wako mnaweza kuona namba yako ya simu kwenye WhatsApp kabla ya kuamilisha akaunti mpya. Unaweza pia kuona picha ya jalada ya mtu mwingine na maelezo yake kuambatana na namba yako ya simu.
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Hii inamaanisha kuwa akaunti ya zamani haikufutwa, na kwa hivyo habari za zamani bado ziko kwenye mfumo. Hii sio maana kwamba mmiliki wa simu anafikia akaunti yako ya WhatsApp utakayo amilisha na namba yako mpya. Mazungumzo yako na data zingine za WhatsApp ziko salama.
Ili kusaidia kuondoa mchanganyiko wa namba za simu zilizotumiwa tena, tunafuatilia akaunti zisizotumiwa. Ikiwa akaunti haitumiki kwa siku 45 na kisha kuanza kutumika kwa kifaa kingine cha rununu, tunachukua hili kama ishara kwamba namba imetumiwa tena. Kwa wakati huu, tutaondoa data ya akaunti ya zamani iliyounganishwa na namba ya simu - kama picha ya jalada na Kuhusu.