Ukipigwa marufuku, utapokea ujumbe huu ndani ya WhatsApp:
“Namba yako ya Simu imepigwa marufuku kutumia WhatsApp. Wasiliana na wasaidizi kwa msaada."
Tambua ya kwamba tunapiga marufuku akaunti ikiwa tunaamini shughuli ya akaunti inakiuka Masharti ya Huduma yetu.
Tafadhali kagua sehemu ya "Matumizi Inayokubalika ya Huduma Yetu" kwenye Masharti ya Huduma kwa uangalifu ili ujifunze zaidi kuhusu matumizi sahihi ya WhatsApp na shughuli zinazokiuka Masharti ya Huduma yetu.
Tunaweza tusitoe onyo kabla ya kupiga marufuku akaunti yako. Ikiwa unadhani akaunti yako ilikuwa imepigwa marufuku kwa makosa, tafadhali tutumie barua pepe na tutaangalia kesi yako.