Jinsi ya kuangalia katalogi
Unaweza kuangalia bidhaa na huduma za biashara kwa urahisi kwenye katalogi ya biashara hiyo. Ikiwa biashara imeunda katalogi, itaonekana kwenye jalada lake la biashara.
Kuangalia katalogi ya biashara
- Fungua soga na biashara hiyo.
- Gusa jina la biashara ili uone jalada la biashara hiyo kwenye WhatsApp Business.
- Gusa ANGALIA ZOTE karibu na KATALOGI.
Au, kama biashara ina katalogi inayotumika, unaweza kugusa kitufe cha ununuzi (
Unaweza pia kuangalia katalogi ya biashara na kuishiriki na ndugu na marafiki katalogi yote au vitu maalumu kwa kuteua mojawapo ya machaguo haya:
- Tuma kiungo kupitia WhatsApp: ili ushiriki kiungo cha bidhaa/katalogi ulizochagua na wengine kwenye WhatsApp
- Nakili kiungo: ili unakili kiungo
- Shiriki kiungo: ili ushiriki bidhaa/katalogi kwa njia ya barua pepe au programu nyingine za kutuma ujumbe
Rasilimali zinazohusiana
Jinsi ya kushiriki bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi: Android | iPhone | Web na Desktop