Jinsi ya kutumia kikapu kwenye WhatsApp Business
Ukiwa mtumiaji wa WhatsApp Business, kipengele cha kikapu kitapatikana kwako kiotomatiki. Ili kutumia kipengele hiki, hakikisha kuwa wewe na wateja wako mnatumia toleo la hivi karibuni zaidi la WhatsApp.
Kipengele hiki kimetengenezwa ili kufanya mchakato wa kuagiza uwe rahisi na wa ufanisi zaidi.
Kutumia au kutotumia vikapu
Ili kuwasha au kuzima kipengele cha vikapu, fungua programu ya WhatsApp. Kisha, malizia hatua zifuatazo:
Android
- Gusa Chaguo zaidi > Zana za Biashara > Katalogi.
- Gusa Chaguo zaidi > Mipangilio.
- Washa Weka kwenye kikapu ili vikapu vionekane kwa wateja wako. Zima Weka kwenye kikapu ili kutotumia kipengele hiki.
iPhone
- Gusa Mipangilio > Zana za biashara > Katalogi.
- Gusa Zaidi > Mipangilio.
- Washa Weka kwenye kikapu ili vikapu vionekane kwa wateja wako. Zima Weka kwenye kikapu ili kutotumia kipengele hiki.
Web/Desktop
- Bofya Zaidi
| juu ya orodha yako ya soga > Katalogi. - Kisha, bofya Zaidi
| > Mipangilio. - Katika sehemu ya Weka kwenye kikapu, bofya Washa kufanya vikapu vionekane kwa wateja wako. Bofya Zima ili kutotumia kipengele hiki.
Kumbuka:
- Wateja hawataweza kulipia bidhaa walizoongeza kwenye vikapu vyao wenyewe.
- Unapobadilisha mipangilio ya vikapu vyako, inaweza kuchukua hadi saa 24 kwa mabadiliko kuonekana. Ikiwa ulizima kipengele cha vikapu, bado unaweza kupokea vikapu kutoka kwa wateja ndani ya muda wa saa 24.