Kipengele cha ombi la maelezo ya akaunti yako kina kuruhusu kuwasilisha ombi la ripoti na kuhamisha ripoti ya maelezo ya akaunti yako ya WhatsApp na mipangilio. Ripoti haitakuwa na ujumbe wako. Kama unahitaji kufikia ujumbe wako kando ya kwenye programu, unaweza kuhamisha historia yako ya soga badala yake.
Tafadhali kumbuka, kipengele hiki hakipatikani kwenye WhatsApp Web na Desktop.
Kimsingi ripoti yako itapatikana siku tatu baada ya tarehe ulipoiomba. Unaweza kurejea tarehe ya Itakuwa tayari unaposubiri ripoti yako.
Dokezo:Mara tu unapoomba ripoti, huwezi kutengua au batilisha ombi lako linalosubiriwa.
Kama ukibadilisha nambari yako ya simu au kufuta akaunti yako, ombi lako linalosubiriwa litabatilishwa na utahitaji kuomba ripoti nyingine.
Wakati ripoti itakapokuwa tayari kupakuliwa, utapokea arifa ya WhatsApp kwenye simu yako, ikisema “Ombi lako la arifa za akaunti sasa linapatikana”. Skrini ya Omba taarifa za akaunti kwenye WhatsApp itakuambia idadi ya muda ulionao kupakua ripoti kabla haijafutwa kutoka kwenye seva zetu. Kwa kuwa ripoti hii ina taarifa zako, kuwa makini kuhusu kuhifadhi, kutuma au kuipakia kwenye huduma zingine.
Baada ya kupakua ripoti kwenye simu yako, utakuwa na chaguo la kufuta moja kwa moja nakala ulilopakua kutoka kwenye simu yako kwa kugusa Futa ripoti > FUTA au Futa ripoti kwenye skrini ya Omba taarifa ya akaunti. Kufuta riporti hakutafuta data yoyote ya akaunti yako ya WhatsApp.