Jinsi ya kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Duka la Facebook
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Duka lako la Facebook huwaruhusu wateja wanaotembelea duka lako kuchagua kukutumia ujumbe wa moja kwa moja kupitia programu ya WhatsApp Business.
Ili kuunganisha akaunti zako, lazima:
- Uwe na akaunti ya WhatsApp Business.
- Uwe msimamizi kwenye akaunti yako ya Kidhibiti cha Biashara cha Facebook.
- Uunganishe Ukurasa wako wa Facebook na Katalogi kwenye akaunti ya Kidhibiti cha Biashara.
- Uwe na ruhusa ya Kudhibiti Ukurasa kwenye Ukurasa wa Facebook na ruhusa ya Kudhibiti Katalogi kwenye Kidhibiti cha Biashara.
Unganisha akaunti yako ya WhatsApp Business kwa duka lako
Kuanza, unda duka kwenye Meneja wa Biashara wa Facebook. Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato huu kwenye makala haya.
Kisha, weka nambari yako ya WhatsApp Business kwenye duka lako na uweke WhatsApp kuwa Njia ya Msingi ya Mawasiliano. Maagizo ya kina kuhusu jinsi ya kukamilisha hatua hizi yanaweza kupatikana kwenye makala haya.