Akaunti ya biashara kwenye WhatsApp inaweza kuorodheshwa kama "Akaunti rasmi ya biashara" au "Akaunti ya biashara" ya kawaida. Biashara haiwezi kuomba au kulipia kuifanya "Akaunti ya biashara" kuwa "Akaunti rasmi ya biashara".
Kwa wakati huu, baadhi ya akaunti za biashara zimeorodheshwa kama "Akaunti rasmi za biashara". Kuorodhesha biashara kama "Akaunti rasmi ya biashara" inategemea vigezo mbalimbali, kwamfano kama chapa inatambulika.
Akaunti yoyote inayotumia programu ya WhatsApp Business itaorodheshwa moja kwa moja kama "Akaunti ya biashara". Biashara zinaweza kusaidia wateja wake kujifunza zaidi kuhusu kampuni zao kwa kujaza maelezo yao ya biashara, ikiwa ni pamoja na tovuti zao za biashara, anwani na masaa ya kazi.