Jinsi ya kubadilisha lugha ya WhatsApp
WhatsApp inapatikana kwa zaidi ya lugha 40 kwenye iPhone na hadi 60 kwenye Android. WhatsApp inafuata lugha ya simu yako. Kwa mfano, ukibadilisha lugha ya simu yako kwa Kihispania, WhatsApp itakuwa kwa Kihispania kiotomatiki.
Badilisha lugha ya simu yako
Android: Nenda kwenye simu yako Mipangilio > Mfumo > Lugha & ingizo > Lugha. Gusa na shikilia lugha kuihamisha juu, au gusa Ongeza lugha
.iPhone: Nenda kwa iPhone Mipangilio
> Jumla > Lugha & Eneo > Lugha ya iPhone. Chagua lugha, kisha gusa Badilisha kuwa {language}.KaiOS: Bonyeza Mipangilio kwenye menyu ya programu > biringiza kwa upande ili kuchagua Ubinafsishaji > biringiza chini na bonyeza Lugha > bonyeza Lugha > chagua lugha unayotaka kutumia > bonyeza SAWA au CHAGUA.
Lugha iliyochaguliwa kwenye simu yako itaonyeshwa kwenye WhatsApp Web.
Hiari hii inapatikana kwa nchi zinazoauniwa
Ikiwa unatumia simu ya Android, unaweza kuwa na hiari ya kubadili lugha ya WhatsApp kutokea ndani ya programu. Ikiwa huoni hiari hii, labda haiauniwi katika nchi yako.
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Hiari zaidi
> Mipangilio > Gusa > Programu ya Lugha. - Chagua lugha unayotaka.