Imeshindwa kuhifadhi majibu ya haraka
Ikiwa huwezi kuhifadhi majibu yako ya haraka, angalia uhakikishe kuwa jibu hilo limefuata masharti yafuatayo ya umbo.
- Idadi ya juu inayokubalika ya kuhifadhi majibu ya haraka ni 50.
- Urefu wa juu wa njia mkato ya jibu la haraka ni herufi 25.
- Njia mkato haziwezi kuwa na nafasi.
- Njia zote mkato lazima zianze kwa mkwaju wa mbele /.
- Idadi ya juu ya maneno msingi yanayoruhusiwa kwa kila jibu la haraka ni tatu.
- Maneno ya msingi hayawezi kuwa na nafasi au herufi yoyote isiyo ya alfabeti au isiyo ya nambari.
- Urefu wa juu wa neno moja la msingi ni herufi 15.