Jalada lako la biashara ni mojawapo ya zana nyingi za biashara katika programu ya WhatsApp Business ambayo itakusaidia kuanzisha uwepo wa biashara rasmi kwenye WhatsApp.
Jalada la biashara hufanya iwe rahisi kwa wateja wako kufikia maelezo muhimu kuhusu kampuni yako, kama vile jina lako la biashara, anwani, jamii, na maelezo. Unaweza pia kujumuisha katalogi ya bidhaa na huduma zako, barua pepe yako ya biashara, na viungo vya tovuti yako na akaunti za mitandao ya kijamii.
Vipengele hivi vya kipekee katika jalada la biashara husaidia kuokoa muda na nishati, ili kukuwezesha kuzingatia mambo ya maana—kuungana na wateja wako na kukuza biashara yako.