Kuhusu kusawazisha WhatsApp Business na Kurasa za Facebook
Unapotumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kuunganisha Ukurasa wako wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business. Unaweza pia kuchagua kusawazisha maelezo ya biashara yaliyo kwenye Ukurasa wako wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business.
Kuunganisha akaunti ya WhatsApp Business, watumiaji lazima wawe na:
- Ukurasa wa Facebook kwa ajili ya biashara yao
- Akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business
- Matoleo ya hivi karibuni ya programu zote mbili kwa ajili ya simu za mkononi
Mara baada ya kuunganisha Ukurasa wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business, unaweza pia kusawazisha maelezo ya biashara yaliyo kwenye Ukurasa huo wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business. Hii ina maana kuwa akaunti yako ya WhatsApp Business itasasishwa na taarifa kutoka kwenye Ukurasa wa Facebook.
Kuwasha usawazishaji kutajaza kiotomatiki sehemu za jalada la biashara yako kwenye programu ya WhatsApp Business kwa kuweka taarifa zifuatazo kutoka kwenye Ukurasa wa Facebook uliounganishwa:
- Saa za kazi
- Anwani
- Maelezo
- Aina
- URL ya tovuti
- Anwani ya barua pepe