Kuhusu kuunganisha WhatsApp Business na Facebook na Instagram
Unaweza kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wa Facebook na/au Jalada la Instagram ili uwape wateja wako njia ya ziada ya kuwasiliana na biashara yako. Ukiwa umeunganisha Ukurasa wa Facebook au Jalada lako la Instagram na akaunti yako ya WhatsApp Business, nambari yako itaonekana kama chaguo la kuwasiliana kwenye Ukurasa wa Facebook na/au Jalada la Instagram iliyounganishwa. Mteja akigusa chaguo hili la kuwasiliana, ataweza kukutumia ujumbe moja kwa moja kwenye WhatsApp.
Mara baada ya kuunganisha Ukurasa wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business, unaweza pia kusawazisha maelezo ya biashara kutoa kwenye Ukurasa huo wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business. Kufanya hivi kutasasisha kiotomatiki jalada lako la WhatsApp Business kwa kuiwekea maelezo kutoka kwenye Ukurasa wa Facebook.