Kuhusu gharama za data ikiranda
WhatsApp inatumia muunganisho wa intaneti uleule kama kuvinjari kwa wavuti na barua pepe kwenye simu yako. Kama unatumia WhatsApp wakati simu yako inaranda, gharama za data zinaweza kutumika. Wasiliana na mtoa huduma wako wa simu kwa taarifa zaidi kuhusu kuranda kwenye nchi zingine.
Kama huna mpango wa data wa kimataifa, tunapendekeza uzime:
- Data ya rununu na data inaranda kukwepa gharama za data ukiranda. Unaweza kutembelea tovuti ya mtoa msaada wako wa kifaa cha mkononi kwa maelekezo.
- Upakuaji kiotomatiki wa midia kwenye muunganisho wa selula na ukiranda ili kuepuka gharama za data.
Rasilimali zinazohusika:
Jinsi ya kusanidi upakuaji kiotomatiki kwenye: Android | iPhone