Kuhusu kubadilisha simu
Unaweza kuhamia aina ile ile ya simu, kama vile Android kwenda kwenye Android au kuhama kwenda kwenye aina tofauti ya simu, kama vile iPhone kwenda kwenye Android.
Kuhamia kwenye aina ile ile ya simu
Kama unahamia kwenye aina ile ile ya simu, unaweza kuwa na chaguo la kuhamisha historia yako ya soga. Pata maelezo zaidi kuhusu kuhamisha historia yako ya soga kwenye Android au iPhone.
Kuhamia kwenye aina tofauti ya simu
Kama unahamia kwenye aina tofauti ya simu:
- Utaendelea kuwa na taarifa za akaunti yako ikiwa ni pamoja na picha yako ya jalada, maelezo ya kuhusu, soga binafsi, soga za vikundi na mipangilio.
- Kuhamisha historia yako ya soga kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine kwa sasa kunapatikana wakati wa kuhamisha kutoka kwenye iPhone hadi kifaa cha Android au kifaa cha Android kwenda kwenye iPhone. Pata maelezo ya jinsi ya kuhama kutoka kwenye iPhone hadi kwenye kifaa cha Android katika makala haya. Pata maelezo ya jinsi ya kuhama kutoka kwenye kifaa cha Android hadi kwenye iPhone katika makala haya.
Kubaki na namba yako ya simu
Pakua WhatsApp kwenye simu yako mpya halafu usajili namba yako ya simu.
Kubadili ili utumie namba mpya ya simu
- Pakua WhatsApp kwenye simu yako mpya kisha usajili namba yako mpya ya simu.
- Futa akaunti yako ya WhatsApp inayohusishwa na namba yako ya zamani ya simu.
Ikiwa ulisahau kufuta akaunti yako inayohusihwa na namba yako ya zamani ya simu na huwezi kuifikia simu yako ya zamani, taarifa zako zote za akaunti zinazohusishwa na namba hiyo ya simu zitafutwa ikiwa mmiliki mpya wa namba yako ya zamani ataanza kutumia WhatsApp kwenye simu mpya baada ya siku 45.
Kumbuka: Ukimpa mtu simu yako au ukirudisha simu yako ya zamani kwa mtoa huduma wa vifaa vya mkononi, hakikisha kuwa umefuta data yako yote mapema, ikiwa ni pamoja na kwenye kadi ya SD, kama ipo. Kufanya hivyo huhakikisha kuwa hakuna data yako ya binafsi, kama vile historia ya soga zako za WhatsApp, itaangukia kwenye mikono ya mtu mwingine.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu kubadilisha nambari za simu
- Jinsi ya kubadilisha namba yako ya simu kwenye: Android | iPhone
- Imeshindwa kubadilisha namba ya simu
- Jinsi ya kuhamisha data yako ya WhatsApp kutoka kwenye iPhone hadi kwenye simu ya Samsung
- Jinsi ya kuhamisha data yako ya WhatsApp kutoka kwenye Android hadi kwenye iPhone