Kipengele cha kubadilisha nambari kina kuruhusu kubadilisha nambari ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya WhatsApp. Kubadilisha nambari yako ya simu kwenye WhatsApp kutaweza:
Unaweza kuchagua kama unataka kuwaarifu waasiliani wako kuhusu mabadiliko ya nambari yako ya simu. Vikundi vyako vya soga vitaarifiwa unapobadilisha nambari yako ya simu bila kijali kama ulichagua kuwaarifu waasiliani wako. Ili uendelee kuungana na waasiliani wako, tunashauri kuwaarifu kuhusu nambari yako mpya ya simu kabla ya kubadilisha nambari za simu na kuwaomba wafanye mabadiliko yoyote ya lazima kwenye vitabu vya anwani za simu zao.
Dokezo: Kama unabadilisha nambari ya simu na unaendelea kutumia simu ileile kwa nambari mpya ya simu, historia yako ya soga itaendelea kuwepo kwenye simu yako.