Kuhusu katalogi
Watumiaji wa programu ya WhatsApp Business wanaweza kuonyesha na kushiriki bidhaa na huduma zao kwa urahisi na wateja kwa kuunda katalogi. Katalogi huonyeshwa kwenye jalada la biashara.
Kila bidhaa au huduma kwenye katalogi ina kichwa cha kipekee pamoja na sehemu za hiari kujaza ambazo ni pamoja na bei, maelezo, kiungo cha tovuti na msimbo wa bidhaa. Vitambulisho hivi hufanya iwe rahisi kwa wateja kutambua bidhaa kwenye orodha. Wamiliki wa biashara wanaweza kupakia hadi bidhaa au huduma 500 kwenye katalogi zao.
Katalogi iliyosasishwa huwawezesha wateja wa sasa na wanaotarajiwa kutafuta bidhaa au huduma za biashara na kuwasiliana na biashara. Wateja wanaweza kuchagua bidhaa au huduma wanayovutiwa nayo na kuishiriki na marafiki zao au kutuma ujumbe kwa biashara kuuliza maswali.
Kushiriki katalogi kunaruhusu biashara ndogo kusambaza katalogi zao na kufikia wateja watarajiwa. Watumiaji wa WhatsApp Business wanaweza kutuma katalogi kamili kwa wateja ambao tayari wanaowasiliana nao. Wanaweza pia kushiriki kiungo chao cha katalogi mahali popote, kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine, hivyo kuwezesha wateja wengi watarajiwa kugundua biashara zao na kutuma ujumbe kwao moja kwa moja kuhusu bidhaa na huduma zao.
Rasilimali zinazohusiana
- Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi kwenye: Android | iPhone| Web na Desktop
- Jinsi ya kuunda na kudhibiti mikusanyiko kwenye katalogi yako: Android | iPhone | Web na Desktop
- Jinsi ya kushiriki bidhaa au huduma na wateja wako: Android | iPhone | Web na Desktop
- Jinsi ya kuangalia katalogi