Kuhusu Kikapu
Ikiwa unatumia Programu ya WhatsApp Business, sasa unaweza kuwasaidia wateja wako kuagiza kwa urahisi kupitia kipengele cha kikapu. Kikapu kinasaidia kutoa njia mpya kwa wateja wako ili waanze kuagiza moja kwa moja, bila kukutumia ujumbe mmoja mmoja kwa kila bidhaa iliyoorodheshwa kwenye katalogi yako.
Wateja wanaotumia programu ya WhatsApp Messenger wataweza kuona kitufe cha ununuzi kando ya jina lako la biashara katika soga yako au wanapotembelea jalada lako la biashara. Kwa kutumia kitufe hiki cha ununuzi, wanaweza kuvinjari katalogi yako na kuweka bidhaa moja kwa moja kwenye vikapu vyao kutoka kwenye katalogi yako.
Pia wataweza kubadilisha idadi ya kila bidhaa iliyo katika kikapu. Baada ya kuongeza, wateja watakuwa na chaguo la kutuma bidhaa zilizo katika vikapu vyao kwenda kwenye akaunti yako ya biashara kama ujumbe wa WhatsApp.
Kipengele hiki kitawaruhusu wateja waliopo:
- kuagiza haraka
- Kuuliza maswali kuhusu bidhaa nyingi kwa wakati mmoja
- kuagiza bidhaa nyingi mara moja
Pakua mchoro huu wenye maelezo kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka bidhaa kwenye kikapu chako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu katalogi
- Jinsi ya kuangalia katalogi
- Jinsi ya kuagiza bidhaa kwa kutumia kikapu kwenye Android | iPhone