Kuhusu kupiga akaunti marufuku
Ikiwa akaunti yako imepigwa marufuku, utaona ujumbe ufuatao unapojaribu kufikia WhatsApp: "Nambari yako ya simu imepigwa marufuku kutumia WhatsApp. Wasiliana na msaada kwa usaidizi."
Huwa tunapiga akaunti marufuku ikiwa tunaamini kuwa shughuli za akaunti zinakiukaMasharti yetu ya Huduma.
Tunapendekeza ukague kwa makini sehemu ya "Matumizi yanayokubalika ya Huduma Zetu" kwenye Masharti yetu ya Huduma ili uelewe zaidi kuhusu matumizi sahihi ya WhatsApp na shughuli zinazokiuka Masharti yetu ya Huduma. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia WhatsApp kwa uwajibikaji kwenye haya makala ya Kituo cha Msaada.
Tafadhali kumbuka, tunaweza tukakosa kutoa onyo kabla ya kupiga akaunti yako marufuku. Kama unadhani akaunti yako ilipigwa marufuku kwa makosa, tafadhali tutumie barua pepe na tutaangalia swali lako.