Mipangilio ya arifa ni pamoja na sauti za Soga za kibinafsi na Kikundi zinazoingia, arifa ndani ya programu, bendera na mwonekano wa ujumbe.
Kuboresha mipangilio yako ya arifa:
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Zaidi
> mipangilio > arifa.
- Hapa una hiari ya:
- Washa na Zima arifa kwa soga za kikundi na kibinafsi.
- Chagua sauti ya arifa kutoka kwa sauti zilizopo kwenye orodha. Kumbuka: Sauti au nyimbo zilizoboreshwa hazipatikani.
- Chagua ikiwa unataka kuona arifa za ujumbe zinazoingia wakati unatumia programu.
- Washa/zima kutikisika.
- Chagua ikiwa unataka kuona maudhui ya ujumbe unaoingia yaonyeshwe kwenye bendera ya arifa. Kumbuka: Hiari hii haipatikani kwenye Windows Phone 7.
- Unaweza pia kusanikisha arifa za Soga za kibinafsi na za Kikundi:
- Fungua soga na gusa Zaidi
> maelezo ya kikundi au maelezo > arifa zilizoboreshwa au tuliza.
Watumiaji wa Windows Phone 8.1 tu
Kwenye Windows Phone Mipangilio > mfumo > arifa+hatua > WhatsApp una hiari ya:
- Kuzima zote sauti za arifa ya jumbe zinazoingia za WhatsApp:
- Chagua hakuna kutoka kwa menyu ya kushuka Sauti ya arifa.
- Onyesha bendera ya arifa inayoonekana kwenye sehemu ya juu ya skrini (kuchagua au kutochagua sanduku).
Kumbuka:
- Mipangilio ya sauti ya arifa inapatikana tu kwa Windows Phone 8 Sasisho 3 (GDR 3) na matoleo mapya ya mfumo wa uendeshaji.
- Sauti ya arifa unayochagua itafanya kazi tu wakati programu inajiendesha kwenye usuli.
- Ili kuamilisha kikamilifu mipangilio yako ya sauti, tafadhali hakikisha kuwa arifa za simu yako hazikuwekwa kwa utulivu au kutikisa tu.