Mtawala yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki mtawala. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya watawala.
Kumbuka: Muumba wa awali wa kikundi hawezi kuondolewa na daima atabaki mtawala isipokuwa aondoke kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki mtawala:
- Fungua soga ya kikundi ya WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye tab ya Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
- Gusa mshiriki unayetaka kumfanya mtawala.
- Gusa Mfanye mtawala wa kikundi.
Kumwondoa mtawala:
- Fungua soga ya kikundi ya WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye tab ya Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
- Gusa mtawala unayetaka kumwondoa.
- Gusa Ondoa kama mtawala.
Kuwafanya washiriki wengi watawala kwa wakati mmoja:
- Fungua soga ya kikundi ya WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye tab ya Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
- Gusa Mipangilio ya kikundi > Hariri watawala wa kikundi.
- Chagua washiriki unaotaka kuwafanya watawala.
- Gusa Imekamilika.
Kuwaondoa watawala wengi kwa wakati mmoja:
- Fungua soga ya kikundi ya WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye tab ya Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
- Gusa Mipangilio ya kikundi > Hariri watawala wa kikundi.
- Usichague watawala unaotaka kuwaondoa.
- Gusa Imekamilika.