Kuhakikisha utoaji wa arifa za WhatsApp, simu yako ni lazima iwe imesanidiwa vizuri.
- Hakikisha kuwa arifa za WhatsApp hazijatulizwa kwenye mipangilio ya WhatsApp na kwa kila soga:
- Fungua WhatsApp, gusa Zaidi
> mipangilio > arifa na hakikisha ujumbe na arifa ya kikundi zimewekwa kwa Washa.
- Fungua soga unayotaka kupokea arifa kutoka > Zaidi
> maelezo ya kikundi au maelezo na hakikisha kuwa soga haijatulizwa.
- Arifa kwenye Windows Phone inahitaji muunganisho imara wa mtandao, ikiwa simu yako ina muunganisho wa intaneti mbaya au ipo kwenye pembezeo au nje ya eneo, inaweza kuchukua muda kabla ya WhatsApp kuweza kuunganishwa kwenye simu yako na kutoa arifa.
- Ikiwa Kihifadhi Betri kimewezeshwa, arifa hazitatolewa ili kuhifadhi betri. Hakikisha kuwa hali-tumizi ya Kihifadhi Betri imezimwa chini ya Windows Phone Mipangilio > mfumo > kihifadhi betri.
- Hakikisha kuwa WhatsApp imebandikwa kwa Anza. Kwa njia hiyo, ikiwa utakosa arifa, bado unaweza kuona jumla ya jumbe zisizosomwa kwenye kidirisha mubashara.
Tafadhali rejea sehemu zifuatazo kwa hatua zaidi za kila mfumo wa uendeshaji:
Windows Phone 7
Hakikisha kilio kimewashwa na sanduku la "Arifa zingine zote" zimechaguliwa chini ya: Windows Phone Mipangilio > mfumo > mdundo + sauti.

Windows Phone 8
- Hakikisha kilio kimewashwa na sanduku la "Arifa zote zingine" zimechaguliwa chini ya Windows Phone Mipangilio > mfumo > mdundo + sauti.
- Hakikisha kuwa WhatsApp inaonyesha hadhi kinaganaga na hadhi ya haraka kwa skrini ya kufunga kwenye: Windows Phone Mipangilio > mfumo > skrini ya kufunga:
- Chini ya Chagua programu ya kuonyesha hadhi kinaganaga, chagua WhatsApp.
- Chini ya Chagua programu ya kuonyesha hadhi haraka, gusa ikoni unayotaka kubadilisha na chagua WhatsApp.

- Hakikisha umesanidisha muunganisho wa Wi-Fi, ili ibaki imewashwa muda wa skrini ukiisha. Nenda kwa Windows Phone Mipangilio > mfumo > Wi-Fi > juu > Weka Wi-Fi imewashwa muda wa skrini ukiisha.

- Hakikisha umezima Zuia data ya mandharinyuma kwenye hisia data. Kufanya hivi, telezesha skrini ya kuanza kwa upande wa kushoto kuona orodha ya programu tumizi > Hisia Data > Mipangilio > Zuia data ya mandharinyuma > Zima.
Windows Phone 8.1
- Hakikisha WhatsApp inaonyesha hadhi kinaganaga na hadhi ya haraka kwa skrini ya kufunga kwenye: Windows Phone Mipangilio > mfumo > skrini ya kufunga:
- Chini ya Chagua programu ya kuonyesha hadhi kinaganaga, chagua WhatsApp.
- Chini ya Chagua programu ya kuonyesha hadhi haraka, gusa ikoni unayotaka kubadilisha na chagua WhatsApp.
- Hakikisha umezima Zuia data ya mandharinyuma kwenye hisia data. Kufanya hivi, telezesha skrini ya kuanza kwa upande wa kushoto kuona orodha ya programu tumizi > Hisia Data > Mipangilio > Zuia data ya mandharinyuma > Zima.
- Nenda kwa Windows Phone Mipangilio > mfumo > mdundo + sauti > simamia sauti za programu > WhatsApp > chagua mipangilio unayotaka.
- Kwenye Windows Phone Mipangilio > mfumo > arifa+hatua > WhatsApp. Hakikisha Onyesha kwenye kituo cha hatua ipo kwenye Washwa.
Tafadhali soma makala hii ikiwa una masuala ya kuunganisha kwa seva ya Taarifa ya Kusukuma.