Ukipenda kuunda vibandiko vyako mwenyewe kwa WhatsApp, unaweza kuzipakia kwenye programu ya Android au iOS. Unaweza kuchapisha programu yako ya kibandiko kama programu nyingine yoyote kwenye Duka la Google Play au Duka la Programu la Apple, na watumiaji ambao hupakua na kusakinisha programu yako wataweza kutuma vibandiko hivi mara moja kutoka ndani ya WhatsApp. Vibandiko kwenye WhatsApp lazima ziwe halali, ziidhinishwe na kukubalika. Jifunze zaidi kuhusu matumizi yanayokubalika ya Masharti ya Huduma yetu.
Tumetoa sampuli za programu na msimbo wa Android na iOS ambao unaotoa njia rahisi ya kuweka kibandiko chako cha mchoro na kuunda programu inayohitaji tu uzoefu mdogo wa kuendeleza au kuandika programu. Waendelezaji wa juu wanaweza pia kuunda programu za kibandiko ya hali ya juu kutumia seti ya API na kiolesura ambazo WhatsApp inawezesha. Tafadhali soma mahitaji hapa chini ya kuunda vibandiko vyako mwenyewe na tazama mafaili ya NISOME yanayohusiana na sampuli za programu kwa seti kamili ya mahitaji na vidokezo unahitaji kuunda programu zako za kibandiko.
Kumbuka: Ili kuzingatia miongozo ya Duka la Programu la Apple wakati wa kuunda programu ya kibandiko cha iOS, hakikisha kuendeleza kiolesura ya kipekee ya mtumiaji (UI) na mtindo wako mwenyewe na usitumie sampuli za programu UI zetu.
Ili kuunda mchoro wako wa kibandiko, vibandiko vyako lazima vitimize mahitaji yafuatayo:
Lazima pia uandae ikoni ambayo itatumiwa kuwakilisha kifurushi chako cha kibandiko kwenye kichagua au trei ya WhatsApp. Picha hii iwe na pikseli 96x96 na lazima iwe chini ya KB 50. Angalia mafaili ya NISOME zinazohusiana na sampuli za programu kwa vidokezo juu ya kupunguza ukubwa wa trei ya ikoni.
Mbali na mahitaji ya hapo juu, tunashauri sana zifuatazo wakati wa kubuni vibandiko vyako:
#FFFFFF
nje ya kila kibandiko. Tazama hii
sampuli hii ya faili ya Photoshop (PSD).
sampuli ya kibandiko
.Kwa habari kuhusu mahitaji ya muundu wa faili na vifaa unavyoweza kutumia kubadilisha mchoro wa kibandiko chako kwa muundo wa faili unaofaa, angalia mafaili ya NISOME zinazohusiana na sampuli za programu.
Ikiwa una maswali au masuala hasa kuhusiana na kuunda vibandiko, tafadhali tutumie barua pepe kwa developers@support.whatsapp.com. Kwa maswali au masuala mengine, tafadhali wasiliana nasi kwa WhatsApp kwa kuenda Mipangilio > Msaada > Wasiliana Nasi.
Vibandiko vinapatikana kwenye toleo la hivi karibuni ya Android na iOS ya WhatsApp. Ikiwa huoni vibandiko, tafadhali hakikisha WhatsApp imesasishwa. Jifunze jinsi ya kutumia vibandiko kwa: Android | iPhone