Kuongeza namba ya simu ya mwasiliani wa kimataifa:
- Fungua kitabu chako cha anwani.
- Unapoongeza namba ya simu ya mwasiliani, anza kwa kuongeza ishara ya jumlisha (+).
- Ingiza msimbo wa nchi, kufuatiwa na namba kamili ya simu.
- Kumbuka: Msimbo wa nchi ni kiambishi cha namba ambacho kinahitajika kuingizwa kabla ya namba kamili ya simu ya kitaifa ili kupiga simu kwa nchi nyingine. Unaweza kutafuta mtandaoni kupata msimbo wa nchi unayohitaji.
Kwa mfano, ikiwa mwasiliani aliyepo Marekani (msimbo wa nchi “1”) ana msimbo wa eneo “408” na namba ya simu "XXX-XXXX", utaingiza +1 408 XXX XXXX.
Kumbuka:
- Hakikisha kuondoa 0 zozote zinazoongoza au misimbo maalum ya kupiga simu.
- Ikiwa una maana ya kuongeza namba ya simu ya eneo (katika nchi) kwa kitabu chako cha anwani ya simu, ingiza namba kama unavyompigia simu mwasiliani wako.
- Namba zote za simu nchini Ajentina (msimbo wa nchi "54") zinapaswa kuwa na "9" kati ya msimbo wa nchi na msimbo wa eneo. Kiambishi "15" lazima kiondolewe namba ya mwisho itakuwa na tarakimu 13 kwa jumla: +54 9 XXX XXX XXXX
- Namba za simu nchini Meksiko (msimbo wa nchi "52") zinahitajika kuwa na "1" baada ya "+52", hata kama ni namba za Nextel.