Kila moja ya soga zako zina msimbo wa usalama inayotumiwa kuthibitisha kuwa simu na jumbe unazotuma kwenye soga zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani, kama msimbo wa QR pamoja na namba ya tarakimu-60. Misimbo hii ni za kipekee kwa kila soga na zinaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba jumbe unazotuma kwenye soga zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo ya wazi zenye kifunguo maalum kinachoshirikiwa kati yako - na usiwe na wasiwasi, sio kifunguo halisi, hiyo huwekwa kwa siri.
Wakati mwingine, misimbo ya usalama inayotumiwa kwenye ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho yanaweza kubadilika. Hii ni kwa sababu wewe au mwasiliani wako alisakinisha upya WhatsApp au kubadilisha simu.
Kupokea arifa wakati misimbo ya usalama yanapobadilika:
Unaweza kuthibitisha kuwa msimbo wa usalama wa mwasiliani wako ni halali. Jifunze ya kufanya hivyo kwenye nakala hii kuhusu ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho.