Kipengele cha Omba maelezo ya akaunti kinakuruhusu kuomba na kusafirisha ripoti ya maelezo ya akaunti yako ya WhatsApp na mipangilio. Mifano ya habari hii ni pamoja na picha yako ya jalada na majina ya kikundi.
Tafadhali elewa kwamba ripoti hii haihusishi jumbe zako. Ikiwa unataka kusafirisha historia yako ya soga badala yake, unaweza kujifunza jinsi kufanya hivyo katika Kituo chetu cha Msaada.
Ripoti yako itapatikana takribani baada ya siku 3 baada ya tarehe uliyoiomba. Unaweza kuangalia tarehe ya Kuwa tayari unaposubiri ripoti yako.
Kumbuka: Wakati ombi la ripoti yako linasubiriwa, baadhi ya vitendo vya akaunti, ikiwa ni pamoja na kufuta akaunti yako, kubadilisha namba yako au kifaa au kuandikisha tena akaunti yako, kutafuta ombi lako. Ombi lako likifutwa, unaweza kuomba ripoti nyingine.
Wakati ripoti inapatikana, utapokea taarifa ya WhatsApp kwenye simu yako inayoelezea: Ripoti ya maelezo ya akaunti yako sasa inapatikana.
Skrini ya Omba maelezo ya akaunti kwenye programu itakueleza muda ulionao kupakua ripoti yako (kama wiki chache) kabla haijafutwa kwenye seva zetu).
Kupakua ripoti yako:
Hutaweza kutazama ripoti uliopakua ndani ya WhatsApp. Chagua programu yoyote ya nje inayoonekana kwenye trei yako ya kushirikisha ili kusafirisha ripoti. Kwa mfano, unaweza kujitumia nakala ya ripoti kwa baruaa pepe. Kwa sababu ripoti yako ina maelezo ya kibinafsi, kuwa makini unapo hifadhi, kutuma au kupakia kwa huduma zozote.
Mara unapoomba ripoti, huwezi kutengua au kusitisha ombi lako linalosubiriwa.
Baada ya kupakua ripoti yako kwenye simu yako, utakuwa na hiari ya kufuta kabisa nakala iliyopakuliwa kutoka kwenye simu yako. Kufuta ripoti hakutafuta data yoyote ya akaunti yako.