Kipengele cha Nyarakisha Soga kinakuruhusu kuficha soga kutoka kwa skrini yako ya Soga na uipate baadaye, ikiwa inahitajika. Unaweza kunyarakisha soga ya kikundi na kibinafsi ili kupanga vizuri mazungumzo yako.
Kumbuka: Kutumia Nyarakisha Soga hakutafuta soga au kucheleza kwenye kadi ya SD.
Sasa soga imenyarakishwa na haitaonekana kwenye skrini ya Soga.
Soga zilizonyarakishwa zitaonekana pia unapopokea ujumbe mpya kutoka kwa mazungumzo hayo.
Jifunze jinsi ya kutumia Nyarakisha Soga kwenye: iPhone | Windows Phone | WhatsApp Web