Simu ya sauti inakuruhusu kupigia waasiliani wako simu ya bure kwa kutumia WhatsApp, hata kama upo kwenye nchi nyingine. Kupiga simu ya sauti kunatumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya dakika za mpango wako wa simu ya mkononi. Gharama za data zinaweza kutumika.
Kupiga simu ya sauti
Fungua soga ya kibinafsi na mwasiliani unayetaka kumpigia simu.
Kama simu yako imefungwa, utaona skrini ya Simu ya sauti ya WhatsApp inaingia wakati mtu fulani anapokupigia simu, utaweza:
Kutelezesha juu ili kukubali kujibu simu.
Kutelezesha juu kukataa kukataa simu.
Kutelezesha juu kujibu kukataa simu na ujumbe wa haraka.
Kama simu yako haikufungwa, utaona ibukizi ya Simu ya sauti inaingia wakati mtu fulani anapokupigia simu, ambapo unaweza kugusa Kataa au Jibu.
Kubadilisha kati ya simu za sauti na simu za video
Kubadilisha kutoka kwa simu ya sauti kuenda kwa simu ya video
Ukiwa kwenye simu ya sauti, gusa Simu ya video > BADILISHA.
Mwasiliani unayempigia ataona ombi la kubadilisha kuenda kwenye simu ya video na anaweza kukubali au kukataa ubadilisho huo.
Badili kutoka kwa simu ya video kwenda kwa simu ya sauti
Ukiwa kwenye simu ya video, gusa Zima Video, itamjulisha mwasiliani kuwa unampigia simu ya video.
Mara mwasiliani akizimapo video yake, simu itabadilishwa na kuwa simu ya sauti.
Dokezo:
Hakikisha kwamba wewe na waasiliani wako muna muunganisho wa Intaneti imara wakati munapiga au kupokea simu za video za kikundi. Ubora wa simu utategemea mwasiliani mwenye muunganisho dhaifu.
Huwezi kufikia nambari za huduma za dharura kupitia WhatsApp kama vile 911 nchini Marekani. Kupiga simu za dharura, lazima ufanye mipango mbadala ya mawasiliano.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kupiga simu ya sauti ya kikundi kwenye: Android | iPhone