Jinsi ya kuthibitisha namba yako ya simu
Mahitaji
- Unaweza kuthibitisha tu namba ya simu unayoimiliki.
- Ni lazima uweze kupokea simu na SMS kwenye namba ya simu unayojaribu kuthibitisha.
- Ni lazima uzime mipangilio yoyote ya kuzuia simu, au vipengele vya kuzuia programu au utendaji.
- Ni lazima uwe na muunganisho wa intaneti unaofanya kazi kupitia data ya simu au Wi-Fi. Ikiwa unatumia mtandao wa ng'ambo au una muunganisho mbaya, huenda uthibitishaji hautafanyika. Jaribu kufungua www.whatsapp.com kwenye kivinjari cha simu yako ili uone kama umeunganishwa kwenye intaneti.
Jinsi ya kuthibitisha
- Weka namba yako ya simu:
- Chagua nchi yako kutoka kwenye orodha kunjuzi. Kufanya hivyo kutajaza kiotomatiki msimbo wa nchi yako upande wa kushoto.
- Weka namba yako ya simu kwenye sanduku upande wa kulia. Usiweke 0 yoyote kabla ya namba yako ya simu.
- Gusa Inayofuata ili kuomba msimbo.
- Weka msimbo wenye tarakimu 6 unaopokea kupitia SMS.
Ikiwa hukupokea msimbo wenye tarakimu 6 kupitia SMS
- Subiri upau wa maendeleo umalize kisha ujaribu tena. Kusubiri kunaweza kuchukua hadi dakika 10.
- Usikisie msimbo la sivyo utafungiwa nje kwa muda fulani.
- Muda ukiisha kabla ya kupokea msimbo, chaguo la kuomba upigiwe simu litaonekana. Chagua Nipigie simu ili kuomba kupigiwa simu. Ukipokea simu, sauti ya kiotomatiki itakuambia msimbo wenye tarakimu 6. Uuweke ili kuthibitisha WhatsApp.
Kumbuka: Kutegemea mtoa huduma wako, unaweza kutozwa gharama ya SMS na simu.
Hatua za utatuaji
Ikiwa una matatizo unapothibitisha, tafadhali jaribu yafuatayo:
- Anzisha simu yako (Kuanzisha simu yako, zima, subiri sekunde 30 kisha uwashe tena).
- Futa kisha usakinishe upya toleo la hivi karibuni la WhatsApp.
- Tuma SMS ya jaribio kutoka kwenye simu yoyote kwenda katika namba yako jinsi ilivyo kwenye WhatsApp, ikiwa na msimbo wa nchi, ili uthibitishe kama unaweza kupokea.
Hatuwezi kukutumia msimbo wako kupitia njia nyingine yoyote kutokana na sababu za usalama.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha kwenye: iPhone