Idadi isiyo sahihi ya beji kwenye ikoni ya WhatsApp inasababishwa na tatizo kwenye simu yako. Tafadhali jaribu hatua hizi ili kuianzisha:
- Muulize mtu akutumie ujumbe mpya wa WhatsApp. Hii lazima ichangamshe idadi ya ujumbe kiotomatiki.
- Gusa na ushikilie kwenye Ikoni ya WhatsApp na ukipeleke kwenye ikoni ya takataka (kawaida iko juu ya skrini), kisha gusa ikoni mpya ya WhatsApp kutoka kwenye dawati lako la programu kwenye skrini yako ya nyumbani.
- Ondoa WhatsApp. Nenda Mipangilio > Kifaa > Programu tumizi > Programu simamizi > Zaidi > Onyesha programu za mfumo > Mtoaji wa Beji > Hifadhi (njia yaweza kua tofauti inategemea simu yako) au kwa programu yako ya idadi ya beji, gusa Futa Data, na kisha sakinisha tena WhatsApp.
- Nenda Mipangilio > Mfumo > Hiari ya msanidi na hakikisha Usiweke shughuli imezimwa. Ikiwa hauna hiari ya msanidi, ruka hii.
- Nenda Mipangilio > Kifaa > Programu tumizi > Programu simamizi > WhatsApp > Hifadhi na gusa Futa Data. Utahitajika kuthibitisha namba yako ya simu wakati mwingine ukifungua WhatsApp.
Idadi ya beji ni utendaji wa taarifa unaotolewa na kizinduzi chako na sio utendaji wa WhatsApp. Ikiwa utaendelea kupata matatizo, tafadhali wasiliana na mtengenezaji wa simu yako.
Tafuta jinsi ya kupata idadi ya beji kwenye programu yako hapa.