Ikiwa unapata matatizo wakati unapopakua au kusasisha WhatsApp kutoka Duka la Google Play, labda ni kwa sababu ya moja ya sababu zifuatazo:
Kama kesi yako haijatajwa hapo juu, tafadhali Kituo cha Msaada cha Google Play kwa hatua maalum za suluhisho.
Misimbo hitilafu
Kwa misimbo hitilafu: 413, 481, 491, 492, 505, 907, 910, 921, 927, 941 na DF-DLA-15
- Ondoa akaunti yako ya Google kwa kupitia Mipangilio ya simu yako. Kisha gusa Watumiaji & akaunti.
- Chagua akaunti yako ya Google na gusa ONDOA AKAUNTI > ONDOA AKAUNTI.
- Anzisha upya simu yako au zima na washa.
- Ongeza tena akaunti yako ya Google kwa kupitia Mipangilio ya simu yako. Kisha gusa Watumiaji & akaunti > Ongeza akaunti > Google.
- Ingia ndani ya akaunti yako ya Google.
- Futa cache ya Hifadhi ya Google Play kwa kwenda kwenye Mipangilio ya simu yako. Kisha gusa Programu & arifa > Maelezo ya programu > Duka la Google Play > Hifadhi > FUTA CACHE.
- Futa data za Duka la Google Play kwa kugusa FUTA DATA > SAWA.
- Jaribu kupakua WhatsApp tena.
Kwa misimbo hitilafu: 101, 498 na 919
Tafadhali fuata maagizo kwenye sehemu "Hakuna hifadhi ya kutosha kwenye kifaa" na jaribu kusakinisha WhatsApp tena.
Kwa misimbo hitilafu: 403, 495, 504, 911, 920, 923, hitilafu za RPC, faili batili, misimbo ya usakinishaji au upakuaji zisizofanikiwa
- Tafadhali fuata maagizo kwenye sehemu "Hakuna hifadhi ya kutosha kwenye kifaa" na hakikisha una hifadhi ya kutosha kwenye kifaa chako.
- Gusa kiungo hiki kutoka kwenye tovuti yetu ili kupakua WhatsApp kama faili ya APK.
- Gusa PAKUA SASA.
- Fungua faili ya APK kuanza kusakinisha.
- Kumbuka: Unapofungua faili ya APK, utahitaji kugusa MIPANGILIO > kubali kutoka kwa chanzo hiki.
Kwa msimbo hitilafu: 490
- Kama unatumia data ya selula, tafadhali pakua, WhatsApp kwenye Wi-Fi tu.
- Kama haifanyi kazi, jaribu yafuatayo:
- Kwenye simu yako nenda Mipangilio > Programuau Programu & arifa > Duka la Google Play > Matumizi ya data > Washa Data za chinichini.
- Kwenye simu yako nenda Mipangilio > Programu au Programu & arifa > Meneja wa Upakuaji > Matumizi ya data > Data za chinichini > Washa Data za chinichini.
- Ikiwa vidokezo vilipo hapo juu havifanyi kazi, jaribu kufuta cache ya Duka la Google Play nenda kwenye Mipangilio ya simu yako. Kisha gusa Programu & arifa > Maelezo ya programu > Duka la Google Play > Hifadhi > Futa cache.
- Futa data za Duka la Google Play kwa kugusa Futa hifadhi > SAWA.
- Jaribu kupakua WhatsApp tena.
Hakuna hifadhi ya kutosha kwenye kifaa
Ikiwa huwezi kusakinisha WhatsApp kutokana na nafasi haitoshi kwenye simu yako, jaribu kufuta cache ya Duka la Google Play na data:
- Kwenye simu yako nenda Mipangilio, kisha gusa Programu & arifa > Maelezo ya programu > Duka la Google Play > Hifadhi > FUTA CACHE.
- Gusa FUTA DATA > SAWA.
- Anzisha upya simu yako, halafu jaribu kusakinisha WhatsApp tena.
Ikiwa bado hauwezi kusakinisha WhatsApp, hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kujenga nafasi ya bure kwenye simu yako:
- Futa cache na data kwa kuenda kwenye Mipangilio > Storage ya simu yako.
- Hamisha data na programu kwa kadi ya SD ya nje.
- Futa programu ambazo hutumii.
- Angalia kwenye folda za WhatsApp hizi hapa chini zilizojificha. Kumbuka unaweza kufikia hizi folda kwa meneja wa faili:
- Folda ya picha inapatikana: /WhatsApp/Media/WhatsApp Picha/Tumwa.
- Folda ya video inapatikana: /WhatsApp/Media/WhatsApp Video/Tumwa.
- Folda ya jumbe za sauti inapatikana: /WhatsApp/Media/WhatsApp Maelezo ya Sauti.
Kima cha chini cha GB 1 ya nafasi ya bure inapendekezwa wakati wa kusakinisha au kusasisha programu.
Kumbuka: Ukifuta picha, video au jumbe za sauti za WhatsApp, hutaweza kuzitazama au kuzisikiliza tena.
Programu hii haipatani na Kifaa chako cha Android
Tafadhali angalia vifaa vyote vinavyotumika katika nakala hii.
Hakipatikana katika nchi yako
Ukiona hitilafu “Hakipatikana katika nchi yako”, au kama vidokezo vya suluhisho kutoka kwa Kituo cha Msaada cha Google Play hazikusaidii, tembelea ukurasa huu kupakua WhatsApp kama faili ya APK na sasisha programu. Unapofungua faili ya APK, utahitaji kugusa MIPANGILIO > kubali kutoka kwa chanzo hiki.