Imeshindwa kuunganisha kwenye WhatsApp
Ikiwa huwezi kutuma au kupokea ujumbe kwenye WhatsApp, huenda huna muunganisho wa intaneti. Ili kuangalia muunganisho wa intaneti wa kifaa chako:
- Angalia kama kuna aikoni ya saa karibu na ujumbe wako badala ya alama ya tiki. Ikiwa ipo, ina maana kwamba ujumbe wako haujawasilishwa.
- Angalia ishara ya mtandao kwenye kifaa chako ili uone ikiwa inamweka au haipo.
Utatuaji
Matatizo mengi ya muunganisho yanaweza kutatuliwa kwa kufanya mojawapo ya yafuatayo:
Mipangilio ya kifaa
- Anzisha kifaa chako upya kwa kukizima na kukiwasha tena.
- Fungua Mipangilio ya kifaa chako > gusa Mtandao na intaneti > washa kisha uzime Hali ya ndegeni.
- Fungua Mipangilio ya kifaa chako > gusa Mtandao na intaneti > Intaneti. Karibu na mtoa huduma wako, gusa aikoni ya Mipangilio. Washa Data ya simu ya mkononi.
- Fungua Mipangilio ya kifaa chako > gusa Programu > WhatsApp > Data ya simu ya mkononi na Wi-Fi > washa Data ya chinichini.
- Sasisha WhatsApp ili utumie toleo jipya zaidi linalopatikana kwenye Duka la Google Play.
- Boresha mfumo wa uendeshaji wa Android kuwa toleo la hivi karibuni linalopatikana kwa kifaa chako.
Mipangilio ya Wi-Fi
- Fungua Mipangilio ya kifaa chako > Mtandao na Intaneti > Intaneti > zima kisha uwashe Wi-Fi.
- Jaribu kuunganisha kwenye mitandao tofauti ya Wi-Fi.
- Hakikisha Wi-Fi inabaki imewashwa wakati upo katika hali tuli.
- Zima kisha uwashe tena ruta yako ya Wi-Fi.
- Wasiliana na kampuni inayokupa huduma za simu na uhakikishe mipangilio yako ya APN imewekwa kwa usahihi.
- Ukiwa unatatizika kuunganisha kwenye WhatsApp unapotumia mtandao wa Wi-Fi ambao kwa kawaida huwa hauutumii, wasiliana na msimamizi wa mtandao huo.
- Hakikisha kuwa hutumii mtandao wa Wi-Fi unaodhibitiwa, kama vile ofisini au katika chuo kikuu. Inawezekana kwamba mtandao wako umewekewa mipangilio ili kuzuia au kupunguza miunganisho.
Mipangilio mingine
- WhatsApp haijaundwa ili kutumiwa kupitia seva mbadala au huduma za VPN. Mipangilio hiyo haiwezi kutumika.
- Zima utumiaji wa mtandao wa nje.
Rasilimali zinazohusiana:
- Imeshindwa kuunganisha WhatsApp: iPhone | KaiOS | WhatsApp Web au Desktop
- Jinsi ya kudhibiti arifa zako