Jinsi ya kutumia hali
Hali hukuruhusu kushiriki masasisho ya maandishi, picha, video na GIF ambazo zitatoweka baada ya saa 24 na pia hufumbwa mwisho hadi mwisho. Ili kutuma na kupokea masasisho ya hali kutoka kwa unaowasiliana nao, wewe na unaowasiliana nao lazima mwe na nambari za simu za kila mmoja wenu zikiwa zimehifadhiwa katika vitabu vya anwani vya simu zenu.
Kuunda na kutuma sasisho la hali
- Fungua WhatsApp > HALI.
- Gusa:
- Maandishi
ili utunge sasisho la hali kwa maandishi. Unaweza kugusa Emoji ili uweke emoji au GIF, T kuchagua fonti, au Rangi kuchagua rangi ya mandharinyuma. - Kamera
au Hali yangu ili upige picha, urekodi video au GIF au uchague picha, video, au GIF iliyopo kutoka kwenye kiteuzi. Unaweza pia kuongeza manukuu au kuhariri picha, video au GIF, pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya.
- Maandishi
- Gusa Tuma
.
Au, unaweza kuunda na kutuma sasisho la hali ikiwa picha, video, au GIF kwa kwenda kwenye kichupo cha SOGA, kisha uguse Kamera
Kumbuka: WhatsApp inaruhusu video zenye muundo wa 3GP na mpeg4.
Kuangalia au kujibu sasisho la hali
- Kuangalia sasisho la hali ya unayewasiliana naye, gusa kichupo cha HALI. Kisha, gusa sasisho la hali ya mhusika.
- Kujibu sasisho la hali ya unayewasiliana naye, gusa JIBU unapoangalia hali.