Kwa viungo vingine unavyopokea kwenye soga, unaweza kuona kiashirio cha kiungo tuhuma.
Kiashirio hiki kinaweza kuonekana kama kiungo kilicho na mchanganyiko wa herufi ambazo huchukuliwa kuwa sio ya kawaida. Watumaji wa barua taka wanaweza kutumia mchanganyiko wa herufi kukudanganya kugusa viungo vinavyoonekana vinaenda kwa tovuti halali, lakini vinakupeleka kwenye tovuti mbovu.
Hapa kuna mfano wa kiungo tuhuma:
https://ẉhatsapp.com/free-tickets
Kumbuka: Herufi ya kwana inaonekana kama herufi “w” laikini badala yake ni herufi "ẉ", ambayo mtumaji wa barua taka amekudanganya ili uzuru tovuti yao ambayo haihusiani na WhatsApp.
Unapopokea, ka makini angalia kwa makini maudhui ya ujumbe. Kama kiungo kimetiwa alama ya tuhuma, unaweza kugusa kiungo na ujumbe ibukizi utatokea, ambayo itaonyesha herufi zisizosawa kwenye kiungo. Kisha unaweza kuchagua kufungua kiungo au kurudi kwenye soga.
WhatsApp kiotomatiki inafanya ukaguzi kuamua kama kiungo ni tuhuma. Ili kulinda faragha yako,, ukaguzi huu hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako, na kwa sababu ya ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, WhatsApp haiwezi kuona maudhui ya jumbe zako.
Kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kukaa salama kwenye WhatsApp, soma nakala hii.