Jinsi ya kuripoti orodha au biashara
Ikiwa unafikiria biashara inakiuka Sera ya Biashara yetu, unaweza kuiripoti.
Ripoti bidhaa au huduma
- Fungua soga na biashara.
- Gusa jina la biashara kuona jalada lao la WhatsApp Business.
- Gusa ONA YOTE karibu na Orodha.
- Gusa bidhaa au huduma kutazama Maelezo.
- Gusa Hiari zaidi
> Ripoti. - Una hiari mbili:
- Kuripoti bidhaa au huduma tu, gusa RIPOTI.
- Kutoa maelezo zaidi, gusa TUELEZE ZAIDI. Kisha, chagua hiari na gusa WASILISHA.
Ripoti biashara
- Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business.
- Gusa Ripoti biashara.
- Una hiari mbili:
- Kuzuia na kuripoti biashara, gusa kisanduku tiki karibu na Zuia mwasiliani na futa jumbe za soga hizi. Kisha, gusa RIPOTI.
- Kuripoti biashara tu, gusa RIPOTI.