Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsAppKituo cha Msaada
WHATSAPP WEB
VIPENGELE
PAKUA
USALAMA
KITUO CHA MSAADA

Chagua lugha yako

  • azərbaycan

  • Afrikaans

  • Bahasa Indonesia

  • Melayu

  • català

  • čeština

  • dansk

  • Deutsch

  • eesti

  • English

  • español

  • français

  • Gaeilge

  • hrvatski

  • italiano

  • Kiswahili

  • latviešu

  • lietuvių

  • magyar

  • Nederlands

  • norsk bokmål

  • o‘zbek

  • Filipino

  • polski

  • Português (Brasil)

  • Português (Portugal)

  • română

  • shqip

  • slovenčina

  • slovenščina

  • suomi

  • svenska

  • Tiếng Việt

  • Türkçe

  • Ελληνικά

  • български

  • қазақ тілі

  • македонски

  • русский

  • српски

  • українська

  • עברית

  • العربية

  • فارسی

  • اردو

  • বাংলা

  • हिन्दी

  • ગુજરાતી

  • ಕನ್ನಡ

  • मराठी

  • ਪੰਜਾਬੀ

  • தமிழ்

  • తెలుగు

  • മലയാളം

  • ไทย

  • 简体中文

  • 繁體中文(台灣)

  • 繁體中文(香港)

  • 日本語

  • 한국어

  • Pakua

  • Vipengele

  • Usalama

  • Kituo cha Msaada

  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
  1. Android
  2. Usalama na Faragha

Jinsi ya kuangalia taarifa za kusomwa

Alama za tiki zitaonekana karibu na kila ujumbe utakaotuma. Kila moja inaashiria yafuatayo:

  • Ujumbe umetumwa.
  • Ujumbe uliwasilishwa kwenye simu ya mpokeaji au vifaa vyake vinginevyo vilivyounganishwa.
  • Mpokeaji amesoma ujumbe.
Kumbuka:
  • Alama ya tiki ya pili itaonekana wakati ujumbe umewasilishwa kwenye kifaa chochote cha mpokeaji kilichounganishwa, hata kama simu yake imezimwa.
  • Katika soga ya kikundi, alama ya tiki ya pili huonekana wakati washiriki wote katika kikundi wamepokea ujumbe wako. Alama za tiki mbili za bluu huonekana wakati washiriki wote katika kikundi wameusoma ujumbe wako.

Maelezo ya ujumbe

Kwa ujumbe wowote unaoutuma, utaweza kuona skrini ya maelezo ya ujumbe, inayoonyesha maelezo ya wakati ujumbe wako uliwasilishwa, kusomwa au kuchezwa na mpokeaji.

Kuona skrini ya maelezo ya ujumbe:

  1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
  2. Gusa na ushikilie ujumbe ulioutuma.
  3. Gusa . Au, unaweza kugusa Chaguo zaidi > Maelezo.

Skrini ya maelezo ya ujumbe huonyesha:

Umewasilishwa:

  • Ujumbe wako umewasilishwa kwenye simu au vifaa vya mpokeaji vilivyounganishwa lakini mpokeaji hajauona.

Umesomwa au Umeonwa:

  • Mpokeaji amesoma ujumbe wako au kuona picha yako, faili ya sauti au video.
  • Mpokeaji ameona ujumbe wako wa sauti, lakini hajaucheza.

Umechezwa:

  • Mpokeaji amecheza ujumbe wako wa sauti.

Kumbuka: Mshiriki anapoondoka kwenye kikundi, skrini ya Maelezo ya ujumbe bado itaonyesha maelezo ya awali ikiwa na washiriki wote, ikiwa ni pamoja na mshiriki ambaye ameondoka kwenye kikundi.

Kukosa taarifa za kusomwa

Ikiwa huoni alama mbili za tiki za bluu, kipaza sauti cha bluu au maandishi "Imefunguliwa" karibu na ujumbe wako uliotumwa au ujumbe wa sauti:

  • Inawezekana kuwa wewe au mpokeaji mmezima taarifa za kusomwa kwenye mipangilio ya faragha.
  • Inawezekana mpokeaji amekuzuia.
  • Inawezekana mpokeaji hajafungua mazungumzo yenu.
  • Inawezekana wewe au mpokeaji mna matatizo ya muunganisho.

Kuzima taarifa za kusomwa

Kuzima taarifa zako za kusomwa, gusa Chaguo zaidi > Mipangilio > Akaunti > Faragha kisha uzime Taarifa za kusomwa.

Kumbuka: Hatua hii haiwezi kuzima taarifa za kusomwa za soga za kikundi au taarifa za kucheza kwa ujumbe wa sauti. Hakuna njia ya kuzima mipangilio hiyo.

Makala haya yamekusaidia?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho si sahihi
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Kituo cha Msaada

WHATSAPP

Vipengele

Usalama

Pakua

WhatsApp Web

Biashara

Faragha

KAMPUNI

Kuhusu

Kazi

Kituo cha Bidhaa

Kuwa karibu

Blog

Hadithi za WhatsApp

PAKUA

Mac/PC

Android

iPhone

MSAADA

Kituo cha Msaada

Twitter

Facebook

Virusi vya Korona

2022 © WhatsApp LLC

Faragha na Masharti