Jinsi ya kuzuia na kuripoti mwasiliani
Unaweza kuacha kupokea ujumbe, simu na masasisho ya hali kutoka kwa waasiliani fulani kwa kuwazuia. Pia unaweza kuwaripoti kama unadhani kuwa wanatuma maudhui yanayotatiza au taka.
Kumzuia mwasiliani
- Fungua WhatsApp, gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio. - Gusa Akaunti > Faragha > Waasiliani waliozuiwa.
- Gusa Ongeza
. - Tafuta au chagua mwasiliani unayetaka kumzuia.
- Gusa Ongeza
Unaweza kutumia mbinu hizi mbadala za kuzuia mwasiliani:
- Fungua soga kati yako na mwasiliani husika, kisha gusa Chaguo zaidi
> Zaidi > Zuia > ZUIA au RIPOTI NA UZUIE, kufanya hivi kutaripoti na kuzuia nambari hiyo. - Fungua soga kati yako na mwasiliani, kisha gusa jina la mwasiliani > Zuia > ZUIA.
Kuzuia nambari ya simu usiyoijua
- Fungua soga ya WhatsApp iliyo na nambari ya simu usiyoijua.
- Gusa ZUIA.
- Gusa ZUIA au RIPOTI NA UZUIE, kufanya hivyo kutaripoti na kuizuia nambari.
Kumbuka:
- Waasiliani waliozuiwa hawataweza tena kukupigia simu au kukutumia ujumbe.
- Masasisho yako ya hali, mara ya mwisho kuonwa, kuwa mtandaoni na mabadiliko yoyote unayofanya kwenye picha yako ya jalada hayataonekana tena kwa waasiliani uliowazuia.
- Kumzuia mtu hakutamwondoa mwasiliani huyu kwenye orodha ya waasiliani, wala hakutakuondoa kwenye orodha iliyo kwenye simu ya mwasiliani huyu. Ili ufute mwasiliani, lazima umfute kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
- Kama una wasiwasi kuwa mwasiliani aliyezuiliwa atajua kuwa umemzuia, tafadhali soma makala haya.
Kuruhusu mwasiliani
- Kwenye WhatsApp, gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio. - Gusa Akaunti > Faragha > Waasiliani waliozuiwa.
- Gusa mwasiliani unayetaka kumruhusu.
- Gusa Ruhusu {mwasiliani}. Wewe na mwasiliani sasa mtaweza kutuma na kupokea ujumbe, simu na masasisho ya hali.
Au, unaweza kutafuta mwasiliani uliyemzuia > gusa na ushikilie mwasiliani > gusa Ruhusu {mwasiliani}.
Kumbuka:
- Ukimruhusu mwasiliani, hutapokea ujumbe wowote, simu au masasisho ya hali yaliyotumwa na mwasiliani huyo wakati alipokuwa amezuiliwa.
- Ukimruhusu mwasiliani au nambari ya simu ambayo ulikuwa hujaihifadhi kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, hutaweza kumrejesha mwasiliani huyo au nambari ya simu kwenye kifaa chako.
Kuripoti mwasiliani
- Fungua soga na mtumiaji unayetaka kumripoti.
- Gusa Chaguo zaidi
> Zaidi > Ripoti.- Weka alama ya tiki kwenye kisanduku ikiwa ungependa pia kumzuia mtumiaji na kufuta ujumbe kwenye soga.
- Gusa RIPOTI.
Kumbuka: Mara baada ya kuripoti, WhatsApp itapokea ujumbe wa hivi karibuni uliotumwa kwako na mtumiaji au kikundi ulichoripoti, pamoja na maelezo kuhusu mtagusano wako wa hivi karibuni na mtumiaji aliyeripotiwa.
Kuripoti picha au video ya kutazama mara moja
- Fungua picha au video ya kutazama mara moja.
- Gusa Chaguo zaidi
> Ripoti mwasiliani.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu kutazama mara moja, soma makala haya.