Jinsi ya kucheza ujumbe za sauti
Ujumbe wa sauti unaopokelewa kwenye WhatsApp hupakuliwa kiotomatiki.
Kwenye ujumbe uliopokelewa utaona:
- Maikrofoni ya kijani
kwenye ujumbe wa sauti ambao hujaucheza. - Maikrofoni ya bluu
kwenye ujumbe wa sauti ambao tayari umeucheza.
Kucheza ujumbe wa sauti
- Gusa Cheza
ili usikilize ujumbe wa sauti ulioutuma au kuupokea. - Kusikiliza ujumbe.
- Kupitia spika za masikioni za simu yako: Shikilia simu kwenye sikio lako ili kucheza ujumbe kupitia spika za masikioni za simu yako.
- Kwenye kipaza sauti cha simu: Shikilia simu mbali na kichwa chako ili kucheza ujumbe kwenye kipaza sauti cha simu.
- Kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani: Ujumbe wa sauti utachezwa kupitia kipokea sauti kinachobanwa kichwani wakati kimeunganishwa na simu.
- Wakati ujumbe unacheza, unaweza kugusa aikoni ya 1x kuongeza kasi kwa hadi mara 1.5 au mara 2.
- Unaweza pia kubonyeza kwa muda nukta iliyo katika mwonekano wa wimbi na kuiburuta hadi kwenye kipima muda cha ujumbe unakotaka kuanza kuucheza.
- Ujumbe wa sauti utaendelea kucheza hata ukienda kwenye soga au kikundi kingine kwenye WhatsApp.
- Unapocheza ujumbe wa sauti halafu uondoke kwenye soga, kichezaji kidogo kitaonekana juu ya skrini yako.
- Unaweza kusitisha, kucheza na kufunga ujumbe wa sauti au kurudi kwenye soga ya awali.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti