Kuhama kutoka kwa WhatsApp Messenger kuenda kwa WhatsApp Business ni haraka, rahisi, na kunaaminika. Tunapendekeza uunde chelezo ya ndani au ya Google Drive ya akaunti yako kabla ya kuanza mchakato wa kuhamisha. Jifunze jinsi ya kuunda chelezo kwenye makala hii.
- Sasisha WhatsApp Messenger na pakua WhatsApp Business kutoka kwa Duka la Google Play.
- Fungua WhatsApp Business.
- Kumbuka: Fungua WhatsApp Business na uiache imefunguliwa na simu imewashwa mpaka mchakato wa uhamisho umekamilika.
- Soma Masharti ya Huduma ya WhatsApp Business. Gusa KUBALI NA ENDELEA kukubali masharti.
- WhatsApp Business hutambua kiotomatiki namba unayotumia katika kwenye WhatsApp Messenger. Kuendelea, gusa hiari ya namba yako ya biashara.
- Ikiwa namba inayoonekana sio namba unayotaka kutumia, gusa TUMIA NAMBA TOFAUTI na pitia njia ya kawaida ya mchakato wa uthibitisho.
- Gusa ENDELEA > RUHUSU kuruhusu WhatsApp Business kufikia historia yako ya soga na media.
- Ingiza msimbo wa tarakimu-6 ya SMS kuthibitisha namba yako.
- Unda jalada lako la biashara > gusa MBELE.
Rasilimali zinazohusiana: