Jinsi ya kukagua msimbo wa QR ya biashara ya WhatsApp
Unaweza kuungana na biashara kwenye WhatsApp kwa urahisi kwa kukagua msimbo yao wa QR ya WhatsApp. Kamera ya WhatsApp inaweza tu kukagua misimbo rasmi ya QR ya WhatsApp.
Kagua msimbo wa QR ya biashara
Kagua kwa kibinafsi
- Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
- Gusa KAGUA MSIMBO.
- Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kuikagua.
- Gusa ENDELEA NA SOGA.
- Gusa ONGEZA kuongeza biashara kama mwasiliani.
Unaweza pia kukagua kwa kamera ya WhatsApp:
- Fungua WhatsApp > gusa Kamera
. - Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kuikagua.
Kagua kutoka kwa Kichanja
- Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
- Gusa KAGUA MSIMBO.
- Gusa aikoni ya Matunzio chini ya skrini.
- Chagua msimbo wa WhatsApp QR kutoka kwa Matunzio au gusa Zaidi
> Picha kuchagua kutoka kwa Picha zako. - Gusa SAWA.
Kagua kutoka kwa kamera ya WhatsApp
- Fungua WhatsApp > gusa Kamera
. - Chagua picha yenye msimbo wa QR wa WhatsApp kuikagua.