Kuongeza vifurushi vya vibandiko, gusa Emoji > Vibandiko > Ongeza.
Gusa Pakua karibu na kifurushi cha vibandiko unachotaka kupakua. Ukiulizwa, gusa PAKUA • {ukubwa wa faili}.
Alama hakikishi ya kijani itatokea mara tu upakuaji utakapokamilika.
Gusa Rudi.
Tafuta na uguse kibandiko unachotaka kutuma.
Baada ya kugusa kibandiko, kitatumwa kiotomatiki.
Hiari zaidi:
Gusa Hivi karibuni ili uone vibandiko ulivyotumia hivi karibuni.
Gusa Vipendwa ili uone vibandiko unavyopendelea.
Kufanya kibandiko kiwe kwenye vipendwa, gusa kibandiko kwenye soga ya binafsi au ya kikundi > ONGEZA KWENYE VIPENDWA. Au, gusa Emoji > Vibandiko. Gusa na ushikilie kibandiko, kisha gusa ONGEZA.
Kuondoa kibandiko kwenye vipendwa, gusa kibandiko husika kwenye soga ya binafsi au ya kikundi > ONDOA KWENYE VIPENDWA. Au, gusa Emoji > Vibandiko > Vipendwa. Gusa na ushikilie kibandiko, kisha gusa ONDOA.
Vibandiko vimewekwa kwenye makundi kwa kutegemea emoji zinazoonekana kwenye aikoni. Gusa kisanduku cha moyo ili uone makundi ya vibandiko.
Gusa Ongeza ili upate machaguo zaidi ya vibandiko. Sogeza mpaka mwisho wa kichupo cha VIBANDIKO VYOTE halafu uguse PATA VIBANDIKO ZAIDI. Kufanya hivyo kutakupeleka kwenye Duka la Google Play, ambapo utaweza kupakua programu za vibandiko.
Gusa Tafuta ili utafute vibandiko mahususi ulivyoovipakua. Unaweza kutafuta vibandiko kwa kutumia maandishi au emoji.
Kumbuka: Vibandiko unavyopakua nje ya WhatsApp huenda visiweze kutafutika ikiwa muundaji wa kibandiko hakufuata miongozo ya WhatsApp ya kuwekea vibandiko lebo.
Utafutaji wa vibandiko hufanyika nje ya mtandao kabisa. WhatsApp haikusanyi taarifa kuhusu utumiaji wako wa utafutaji wa vibandiko au maneno ya msingi unayotumia wakati wa kutafuta vibandiko.
Ili uone vifurushi vya vibandiko ambavyo umepakua, gusa Ongeza > VIBANDIKO VYANGU.
Kama unataka kufuta kifurushi fulani cha vibandiko, gusa Futa > FUTA. *Ili upange upya vibandiko vyako, gusa na uburute Panga upya karibu na kifurushi cha vibandiko.
Ili usasishe vifurushi vya vibandiko, gusa Ongeza pindi kitone cha kijani kikitokea. Kwenye kichupo cha VIBANDIKO VYOTE, gusa SASISHA karibu na vifurushi vya vibandiko vinavyohitaji kusasishwa. Ukiulizwa, gusa SASISHA • {ukubwa wa faili}.
Alama hakikishi ya kijani itatokea mara tu sashisho itakapokamilika.
Vibandiko vinapatikana kwenye matoleo ya hivi karibuni ya WhatsApp. Kama huoni vibandiko, hakikisha unasasisha ili upate toleo jipya zaidi la WhatsApp kwenye duka la programu la simu yako.