Jinsi ya kuweka au kuondoa nyota kwenye ujumbe
Kipengele cha jumbe zenye nyota kinakuruhusu kuziwekea ala jumbe maalum ili uweze kuzirejea haraka tena baadaye.
Weka nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe unaotaka kuuwekea nyota.
- Gusa Nyota
.
Kuondoa nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe wenye nyota.
- Gusa Ondoa nyota
.
Kumbuka: Kuondoa nyota hakutafuta ujumbe.
Angalia orodha ya jumbe ulizoziwekea nyota
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Hiari zaidi
. - Gusa Jumbe zenye nyota.