Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na watu pamoja na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Kwa hivyo, ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Kutuma ujumbe wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie maikrofoni
halafu uanze kuzungumza. - Mara unapomaliza, ondoa kidole chako kwenye maikrofoni
. Ujumbe wa sauti utatumwa kiotomatiki.
Wakati unanakili ujumbe wa sauti, unaweza kutelezesha kidole kushoto ili kughairi.
Kutuma ujumbe mrefu zaidi wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie maikrofoni
halafu uanze kuzungumza. - Telezesha kidole juu ili uanze kurekodi bila kushika.
Unaweza pia kugusa kitufe chekundu cha kusitisha
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
- Maikrofoni ya kijivu
kwa ujumbe wa sauti ambao haujachezwa na wapokeaji wote (lakini unaweza kuwa umechezwa na baadhi). - Maikrofoni ya bluu
kwa ujumbe wa sauti ambao wapokeaji wote wameucheza.
Kumbuka: Kwenye baadhi ya simu, huenda itakubidi usubiri sekunde moja kabla ya kuzungumza ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haurekodiwi.