Jinsi ya kutuma miitikio ya ujumbe
Unaweza kuitikia ujumbe katika soga zako binafsi na za kikundi ukitumia emoji. Unaweza kuona miitikio yote kwenye ujumbe kwa kugusa emoji ya miitikio chini ya ujumbe husika.
Kumbuka:
- Unaweza kuweka mwitikio mmoja tu kwa kila ujumbe.
- Miitikio kwenye ujumbe unaotoweka itatoweka wakati ujumbe husika unatoweka.
- Haiwezekani kuficha miitikio au idadi ya miitikio.
- Wapokeaji wanaweza kuona mwitikio wako kabla hujauondoa au kama uondoaji hakufaulu. Hutaarifiwa ikiwa uondoaji wa mwitikio haujafanyika.
Kuweka mwitikio kwenye ujumbe
Unapoweka mwitikio, ni mtumaji wa ujumbe unaoitikia pekee ndiye atapokea arifa.
- Bonyeza ujumbe kwa muda mrefu.
- Gusa ili uchague mojawapo ya emoji zinazoonekana.
Kubadili mwitikio wako
Unaweza kubadilisha mwitikio wako kuwa mwingine.
- Bonyeza kwa muda mrefu ujumbe uliouitikia.
- Gusa emoji tofauti.
Kuondoa mwitiko
Unaweza kuondoa mwitiko wako kwenye ujumbe. Arifa haitatumwa kwa mtumaji wa ujumbe ikiwa utaondoa mwitiko.
- Bonyeza kwa muda mrefu ujumbe uliouitika au gusa mwitikio.
- Gusa emoji uliyoitika nayo ili uiondoe.