Jinsi ya kutuma maudhui
Kushirikisha maudhui, nyaraka, mahali au anwani
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa Ambatisha
. Kisha, gusa:- Hati ili uchague waraka kutoka kwenye simu yako.
- Kamera ili upige picha kwa kamera yako.
- Matunzio ili uchague picha iliyopo au video kutoka kwenye simu yako. Gusa na shikilia ili kuchagua picha nyingi.
- Sauti ili utume sauti iliyopo kutoka kwenye simu yako.
- Mahali ili kutuma mahali au sehemu za karibu.
- Anwani ili utume taarifa ya mawasiliano uliyohifadhi kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kupitia WhatsApp.
- Unaweza pia kuongeza maelezo mafupi kwenye picha na video. Telezesha kati ya picha ili uandike maelezo kwa kila mojawapo.
- Gusa Tuma
.
Kumbuka: Ukubwa wa waraka unaoruhusiwa ni MB 100. Ili kutuma nyaraka kutoka ndani ya WhatsApp, waraka lazima ihifadhiwe ndani ya simu yako. Au, WhatsApp itaonekana kama chaguo la kutuma kwenye menyu ya kushiriki ya programu ambazo zinashughulikia nyaraka. Unapopakua waraka, itahifadhiwa kiotomatiki kwenye folda yako ya Nyaraka za WhatsApp: WhatsApp/Media/WhatsApp Documents, unayoweza kuifikia kwa kutumia programu ya kufungua faili.
Kusambaza maudhui, nyaraka, mahali au anwani
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie aina ya ujumbe unaotaka kusambaza. Unaweza kuchagua zaidi ya ujumbe mmoja.
- Gusa Sambaza
. - Chagua soga unayotaka kusambazia ujumbe.
- Gusa Tuma
.
Unaposambaza maudhui, nyaraka, mahali au anwani, huna haja ya kupakua tena. Ujumbe wowote ambao kwa asili haukutumwa na wewe utakuwa na maandishi "Ulisambazwa".
Kumbuka: Maelezo hayatasambazwa pamoja na maudhui. Hutaweza kusambaza ujumbe kwa orodha ya tangazo.