Jinsi ya kutafuta kwenye WhatsApp
Unaweza kutafuta kwenye soga kwa urahisi ujumbe, picha, video, viungo, GIF, sauti na nyaraka kwa kutumia kipengele cha utafutaji wa WhatsApp.
Tafuta soga na neno msingi
Kipengele cha utafutaji kinakuruhusu kutafuta soga yako kwenye kifaa chako na neno msingi.
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Tafuta
. - Andika neno au kifungu unachotafuta kwenye uga wa Utafutaji.
- Gusa matokeo kufungua ujumbe kwenye hiyo soga.
Tafuta midia na vichujio
Unaweza pia kutafuta soga zako kwa midia kama vile picha, video, viungo, GIF sauti na nyaraka, kwa kutumia vichujio kwenye kipengele cha utafutaji.
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Tafuta
. - Andika neno au kifungu unachotafuta kwenye uga wa Utafutaji.
- Chagua aina ya midia unayotaka kutafuta.
- Gusa matokeo kufungua ujumbe kwenye hiyo soga.
Chuja midia kwa aina ya maudhui
Unaweza kutazama picha, video, viungo, GIF, sauti au nyaraka zote.
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Tafuta
. - Gusa Picha, Video, Viungo, GIF, Sauti, au Nyaraka kutazama midia kwenye kundi hilo.