Soga zako za WhatsApp zinachelezwa kiotomatiki na kuhifadhiwa kila siku kwenye kumbukumbu ya simu yako. Kutegemea na mipangilio yako, pia unaweza kucheleza mara kwa mara soga zako za WhatsApp kwa Google Drive. Ukiondoa WhatsApp kutoka kwenye simu yako, lakini hutaki kupoteza jumbe zozote, hakikisha unachelezesha au kusafirisha soga zako kabla ya kuondoa.
Nenda WhatsApp > gusa Hiari zaidi
Unaweza kutumia kipengele cha kuhamisha soga ili kuhamisha nakala ya historia ya soga kutoka kwa soga ya kibinafsi au kikundi.
Dondoo: Kipengele hiki hakiwezeshwi Ujerumani.
Barua pepe itaundwa na historia yako ya soga iliyoambatishwa kama nyaraka ya .txt.
Dondoo:
Jinsi ya kurejesha historia ya soga yako
Jinsi ya kucheleza kwa Google Drive