Unaweza kuhamisha data yako ya WhatsApp kwenye simu mpya kwa kurejesha kutoka kwenye Google Drive au chelezo ya ndani.
Kurejesha kutoka chelezo ya Google Drive
Ili kufanikiwa kurejesha chelezo ya Google Drive, unahitaji kutumia nambari hiyo ya simu na akaunti ya Google iliyotumika kuunda chelezo.
Kurejesha chelezo yako:
Ondoa na sakinisha upya WhatsApp.
Fungua WhatsApp na thibitisha nambari yako.
Ukiulizwa gusa REJESHA kurejesha soga zako na media kutoka kwa Google Drive.
Baada ya mchakato kukamilika, gusa MBELE. Soga zako zitaonyeshwa mara uanzishaji ukikamilika.
WhatsApp itaanza kurejesha faili zako za media baada ya kurejesha soga zako.
Ikiwa unasakinisha WhatsApp bila chelezo zozote za awali kutoka Google Drive, WhatsApp itarejesha kiotomatiki kutoka kwa faili lako la chelezo la ndani.
Kurejesha chelezo la ndani
Ikiwa unataka kutumia chelezo ya ndani, utahitaji kuhamisha faili kwenye simu mpya kwa kutumia kompyuta, uchunguzi wa faili au kadi ya SD.
Dondoo:
Simu yako itahifadhi hadi kiasi ya siku saba za faili za chelezo za ndani.
Chelezo za ndani zinaundwa kiotomatiki kila siku saa nane asubuhi (2:00AM) na kuhifadhiwa kama faili kwenye simu yako.
Ikiwa data yako haijahifadhiwa kwenye folda ya /sdcard/WhatsApp/, unaweza kuona folda za "internal storage" au "main storage".
Rejesha chelezo ya ndani ambayo sio ya hivi karibuni
Ikiwa unataka kurejesha chelezo ya ndani ambayo sio ya hivi karibuni, utahitaji kufanya yafuatayo:
Pakua programu ya kusimamia faili.
Kwenye programu ya kusimamia faili, nenda kwa sdcard/WhatsApp/Databases. Ikiwa data yako haijahifadhiwa kwenye kadi ya SD, unaweza kuona "internal storage" au "main storage" badala ya sdcard.
Badilisha jina la faili la chelezo kutoka msgstore-YYYY-MM-DD.1.db.crypt12 kuwa msgstore.db.crypt12. Inawezekana kwamba chelezo ya awali inaweza kuwa kwenye itifaki ya awali, kama crypt9 au crypt10. Usibadilishe nambari ya kiendelezi cha crypt.