Mapendeleo ya arifa yanaweza kusimamiwa kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Badilisha mipangilio ya arifa ya WhatsApp
Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Arifa.
Hapa unaweza kubadilisha arifa za jumbe, vikundi, na simu kwa kuchagua:
Ikiwa ni kuweka milio wa mazungumzo kwa jumbe zinazoingia na kuondoka kuwasha au kuzima.
Mlio wa arifa au mwito.
Muda wa mtikiso.
Kama unaweza kuonyesha arifa za ibukizi kwenye Android 9 na zaidi. Hii inaruhusu arifa kuonekana katikati ya skrini yako.
Rangi nyepesi ya arifu kwa simu zinazowezeshwa.
Ikiwa utatumia arifa za kipaumbele cha juu kwenye Android 5 na mpya zaidi. Hii inaonyesha mwonekano wa arifa juu ya skrini yako na inaweza kutumika kulemaza arifa za kuchungulia.
Kumbuka: Kuzima arifa za kipaumbele kutasababisha arifa za WhatsApp kuwekwa chini kwenye skrini yako.
Kuanzisha mipangilio yako ya arifa, gusa Mipangilio > Arifa > gusa Hiari zaidi> Mipangilio ya arifa ya kuanzisha > ANZISHA.
Geuza arifa
Unaweza kugeuza arifa kwa kuchagua hiari tofauti kwa mlio, mtetemo, ibukizi na mwanga:
Kufungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
Gusa Arifa za kipekee > weka alama Tumia arifa za kipekee.
Nyamazisha arifa
Kufungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
Gusa Nyamazisha arifa.
Chagua muda ambao ungependa kutuliza arifa halafu gusa SAWA.
Mbadala, ondoa alama ya tiki kwenye Onyesha arifa kuzuia arifa kuonekana.