Jinsi ya kudhibiti arifa zako
Mapendeleo ya arifa yanaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Kubadili mipangilio ya arifa za WhatsApp
Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
Unaweza kubadilisha arifa za ujumbe, vikundi na simu kwa kuchagua:
- Iwapo unataka kuwasha au kuzima milio kwa ujumbe unaoingia na unaotumwa.
- Mlio au toni ya arifa.
- Muda wa mtikisiko.
- Iwapo unataka kuonyesha arifa ibukizi kwenye vifaa vya Android 9 na matoleo ya zamani. Hatua hii huruhusu arifa kuonekana katikati ya skrini yako.
- Rangi ya mwanga wa arifa kwa simu zinazoruhusu kubadilisha.
- Iwapo utatumia arifa za kipaumbele cha juu kwenye Android 5 na matoleo mapya zaidi. Hatua hii huonyesha muhtasari wa arifa juu ya skrini yako na inaweza kutumika kuzima arifa za kuchungulia.
Kumbuka: Kuzima arifa za kipaumbele cha juu kutasababisha arifa za WhatsApp zionyeshwe katika sehemu ya chini kwenye skrini yako.
Ili uweke upya mipangilio ya arifa, gusa Mipangilio > Arifa > gusa Chaguo zaidi
Kuweka arifa upendavyo
Unaweza kuweka arifa upendavyo kwa kuteua chaguo tofauti za mlio, mtetemo, arifa ibukizi na mwanga:
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
- Gusa Arifa maalum > wekea alama Tumia arifa maalum.
Kumbuka: Simu za kikundi hutumia mlio chaguomsingi wa simu. Mlio huu wa simu hauwezi kuwekewa mapendeleo.
Kuzima arifa
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
- Gusa Zima arifa.
- Chagua kipindi cha muda ambao ungependa kuzima arifa kisha uguse SAWA.
Au, ondoa alama ya tiki kwenye Onyesha arifa ili uzuie arifa zisionekane.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuzima au kuwasha arifa: iPhone | Web na Desktop | KaiOS