Jinsi ya kusimamia wasimamizi wa kikundi
Msimamizi yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki awe msimamizi. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya wasimamizi. Mtu aliyeanzisha kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa aondoke kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
> Maelezo ya kikundi.

- Gusa mshiriki unayetaka kumfanya msimamizi.
- Gusa Mfanye msimamizi wa kikundi.
Kuwafanya washiriki wengi kuwa wasimamizi kwa wakati mmoja
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
> Maelezo ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
- Gusa Mipangilio ya kikundi > Hariri wasimamizi wa kikundi.
- Chagua washiriki unaotaka kuwafanya wasimamizi.
- Gusa alama ya tiki ya kijani unapomaliza.
Kuondoa msimamizi
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
> Maelezo ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
- Gusa msimamizi unayetaka kumwondoa.
- Gusa Mwondoe kuwa msimamizi.
Kuwaondoa wasimamizi wengi kwa wakati mmoja
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
> Maelezo ya kikundi.
- Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Hiari zaidi
- Gusa Mipangilio ya kikundi > Hariri wasimamizi wa kikundi.
- Ondoa tiki kwenye wasimamizi unaotaka kuwaondoa.